BRUSSELS : Marekani inahitaji Ulaya imara
22 Februari 2005Rais George W Bush wa Marekani ameanza ziara ya kurekebisha uhusiano na Ulaya kwa kutowa hotuba kuu mjini Brussels Ubelgiji.
Akizungumza mwanzoni mwa ziara yake ya siku tano Rais Bush amesema Marekani inahitaji Ulaya ilio imara ili kujenga amani ya dunia.Rais huyo wa Marekani anawasilisha ujumbe wake huo wa ushirikiano mpya kati ya Marekani na Ulaya kwenye mikutano ya viongozi na Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO na Umoja wa Ulaya leo hii na kuwa na mazungumzo katika nyakati tafauti na viongozi wa mataifa 26 wanachama wa NATO na mataifa 25 yanayounda Umoja wa Ulaya.
Katika hotuba yake ya ufunguzi hapo jana Bush aligusia suala la Iran na kusema nchi hiyo haipaswi kuachiliwa itengeneze silaha za nuklea lakini ameongeza kusema kwamba shinikizo la kidiplomasia kwa Iran bado lingaliko katika hatua za awali.
Rais Bush pia ameitaka Syria kuondowa wanajeshi kutoka Lebanon.