Brussels: Jumuiya ya Ulaya itatuma wachunguzi 200 kuusimamia mkataba wa amani wa Aceh, huko Indonesia
19 Julai 2005Jumuiya ya Ulaya inasema inapanga kutuma wachunguzi 200 kuangalia namna mapatano ya amani katika jimbo la Aceh la Indonesia yatakavotekelezwa. Baada ya kupita miongo mitatu ya vita, chama cha waasi wa Aceh na serekali ya Indonesia zimetangaza rami mapatano ya amani yatakayoanza kufanya kazi Agosti 15. Waangalizi 200 wa Jumuiya ya Ulaya watapelekwa huko, ukiwa ujumbe wa kwanza wa aina hiyo kutumwa na jumuiya katika Asia. Mratibu mkuu wa siasa za kigeni za Jumuiya ya Ulaya, Javier Solana, aliuwambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba Jumuiya ya Ulaya imeombwa na pande zote mbili kuusimamia mkataba huo wa amani ambao pia utaangalia namna unavotekelezwa na nchi tano kutoka Jumuiya ya nchi za Kusini mashariki ya Asia, ASEAN, Malaysia, Singapore, Thailand, Philippines na Brunei.