Brussels. Javier Solana aipongeza serikali mpya ya Kirgistan.
29 Machi 2005Matangazo
Mkuu wa sera za mambo ya kigeni katika jumuiya ya Ulaya Bwana Javier Solana ameunga mkono serikali mpya ya Kirgistan na kuitaka kuendeleza demokrasia. Bwana Solana amemtaka kiongozi wa mpito Bwana Kurmanbek bakiyev kuingia katika majadiliano na serikali ya zamani. Bunge jipya limemteua kiongozi wa upinzani Bwana bakiyev kuwa waziri mkuu pamoja na wadhifa wa kaimu rais baada ya siku kadha za maandamano dhidi ya kile kinachotuhumiwa kuwa ni wizi wa kura katika uchaguzi mkuu.