BRUSSELS: Iran isianzishe upya mradi wa kuimarisha uranium
24 Mei 2005Matangazo
Umoja wa Ulaya kwa mara nyingine tena umeionya Iran kuwa isianze kuimarisha madini ya uranium.Vile vile Umoja huo umesema kuwa uhusiano wao unategemea vile serikali ya Tehran itakavyotimiza wajibu wake wa kusitisha mradi huo.Onyo hilo limetolewa siku mbili kabla ya kufunguliwa majadiliano muhimu mjini Geneva kati ya Iran na wanachama watatu wa Umoja wa Ulaya yaani Ujerumani,Uingereza na Ufaransa kuhusu mradi wa kinuklia wa Iran.