BRUSSELS: Hisia za kimataifa kuhusu uchaguzi wa rais wa Iran
27 Juni 2005Matangazo
Kuchaguliwa kwa Mahmoud Ahmadinejad kama rais mpya wa Iran kumezusha hisia mbali mbali katika jumuiya ya kimataifa.Mkuu wa Umoja wa Ulaya kuhusu masuala ya haki na usalama,Franco Frattini amesema,wapenda mageuzi nchini Iran wamepata ushinde wa shaka.Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Joschka Fischer pia ameeleza wasi wasi kuhusu utaratibu wa uchaguzi wa rais.Miongoni mwa mambo mengine,idadi fulani ya wagombea uchaguzi walipigwa marufuku.Washington kwa upande wake imesema,Iran inakwenda vingine kulinganishwa na nchi za eneo hilo.Israel nayo imeihimiza jumuiya ya kimataifa iwe na siasa moja na iliyo imara kuhusu Iran.