Brussels. Hali ya jela ya Guantanamo bay si ya kibinadamu na ni kinyume cha sheria, lasema baraza la Ulaya.
26 Aprili 2005Matangazo
Baraza la Ulaya limeishutumu Marekani juu ya hali ya jela walimofungiwa watu katika kituo cha kijeshi la Guantanamo nchini Cuba. Katika azimio baraza hilo linye makao yake makuu mjini Strasbourg limesema kuwa hali katika jela hiyo si ya kibinadamu na ni kinyume na sheria.
Bunge hilo limeitaka serikali ya rais Bush katika vita vyake dhidi ya ugaidi kuheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria.