Brussels. Baadhi ya mataifa ya Ulaya, yapinga kulegezwa masharti ya huduma za ndani ya nchi
23 Machi 2005Matangazo
.
Viongozi wa jumuiya ya Ulaya wanaokutana mjini Brussels wamejadili pendekezo la kulegeza masharti ya sekta ya huduma za ndani katika mataifa hayo. Lakini mataifa wanachama yamesema kuwa agizo hilo katika hali yake ya sasa hakidhi taratibu za jumuiya hiyo. Sehemu ya mwanzo ya agizo hilo lijulikanalo kama Bolkestein litazifanya kampuni zinazotoa huduma katika nchi za jumuiya ya Ulaya kubanwa na taratibu katika nchi zao. Hii imeamsha hofu katika mataifa kadha, hasa Ujerumani na Ufaransa kuwa wataingia wafanyakazi ambao watakubali malipo madogo kwa kazi zao kutoka Ulaya ya mashariki.