Brussels. Afrika yaahidiwa misaada.
14 Julai 2006Matangazo
Umoja wa Ulaya umeahidi kutoa zaidi ya Euro bilioni tano kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya miundo mbinu katika bara la Afrika.
Kamishna wa maendeleo wa umoja wa Ulaya Louis Michel amesema kuwa fedha hizo zitatumika kuanzia mwaka 2008 – 2013 kuweza kuisaidia Afrika kuimarisha huduma zake pamoja na miundo mbinu, na kulipa bara hilo msukumo unaohitajika wa kiuchumi.
Mipango inayolenga katika kutoa huduma bora za afya, maji safi na mawasiliano itazinduliwa katika nchi kuazia Senegal hadi Namibia.