BRICS: Tunalaani mashambulizi dhidi ya Iran na Gaza
7 Julai 2025Viongozi wa kundi la BRICS la mataifa yanayoendelea yamelaani mashambulizi dhidi ya Gaza na Iran na kutoa wito wa mageuzi ya taasisi za kimataifa na kuiwasilisha kambi hiyo kama kimbilio la diplomasia ya kimataifa katikati mwa mizozo inayoendelea na vita vya kibiashara duniani.
Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na viongozi hao wameyaita mashambulizi dhidi ya raia wa Iran, miundombinu na vifaa vya nyuklia kama ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa.
Kundi hilo limeonyesha pia wasiwasi mkubwa na kulaani juu ya mashambulizi ya Israel yanayoendelea katika ukanda wa Gaza.
Mkutano huo wa kilele wa siku mbili huko Rio de Janeiro,Brazil ulioanza siku ya Jumapili umezungumzia pia matumizi ya Akili ya kubuni AI na kutoa wito wa kuwepo kwa ulinzi dhidi ya matumizi holela ya teknolojia hiyo.