Kiongozi wa kijeshi Nguema ashangilia ushindi Gabon
14 Aprili 2025Kiongozi wa kijeshi wa Gabon, Brice Oligui Nguema, ashangilia ushindi mkubwa katika uchaguzi wa rais, baada ya matokeo ya awali ya uchaguzi huo jana Jumapili kuonesha amechaguliwa na asilimia 90.35 ya wapiga kura.
Waziri wa mambo ya ndani, Hermann Immongault, awali aliweka wazi kwamba Nguema ataongoza muhula wa miaka saba kwa kupata ushindi, baada ya kuchaguliwa na zaidi ya wapiga kura 575,200 kati ya kura zilizohesabiwa hadi sasa katika nchi hiyo ya wakaazi milioni 2.3.Soma pia: Wananchi wa Gabon wanapiga kura kumchagua Rais mpya
Mpinzani wake mkubwa kwenye uchaguzi huo wa Jumamosi alikuwa Alain-Claude Billie By Nze aliyetangazwa kupata asilimia tatu na wagombea wengine sita wakishindwa kupata zaidi ya asilimia 1.
Soma pia: Raia wa Gabon wapiga kura ya maoni kuhusu katiba mpyaNguema ambaye Agosti mwaka 2023 aliuondowa kwa nguvu madarakani utawala wa zaidi ya miongo mitano ulioshikiliwa na Familia ya Bongo, alikuwa akiongoza serikali ya mpito na aliahidi kuirudisha nchi hiyo katika utawala wa kiraia.