You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Brexit
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Umoja wa Ulaya kuisaidia Mali kijeshi
Umoja wa Ulaya unafanya mchakato wa kuanzisha jeshi la kuaminika nchini Mali, ambako waasi wenye itikadi kali ya Kiislamu wamelidhibiti eneo la kaskazini baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini humo.
Taasisi ya kuchunguza benki za Ulaya kuundwa
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuziweka benki zote za bara la Ulaya chini ya taasisi moja ya uchunguzi mwaka ujao, lakini wakashindwa kutangaza tarehe kamili ya kuanza mpango huo.
Scotland sasa kupiga kura ya maoni 2014
Waziri Mkuu wa Uingereza na waziri kiongozi wa Scotland wameanza kampeni ya miaka miwili kuelekea kura ya maoni itakayoamua hatima ya Scotland kuendelea kubakia sehemu ya Uingereza au kujitenga na kuwa taifa huru.
Umoja wa Ulaya wazidisha vikwazo dhidi ya Syria
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya wametangaza vikwazo vipya dhidi ya utawala wa Rais Bashar al-Assad wa Syria, kuzitaifisha mali zake na kuwawekea vikwazo vya kusafiri Wasyria 28.
Wazee wa Mau Mau kuishtaki serikali ya Uingereza
Mahakama nchini Uingereza imepitisha uamuzi kwamba wazee watatu wa Kenya walioteswa na utawala wa Uingereza katika miaka ya 1950 wanaweza kuendeleza madai yao dhidi ya serikali ya Uingereza.
Umoja wa Ulaya watafakari msaada kwa Mali
Umoja wa Ulaya unatafakari namna ya kuisaidia Mali kupambana na wanamgambo wa kiislamu wanaodhibiti sehemu ya Mali kaskazini, baada ya kupokea maombi ya msaada kutoka kwa serikali ya nchi hiyo.
Assad awaambia waasi kamwe hawatamshinda
Mapigano makali yameripotiwa alfajiri ya leo katika miji kadhaa ya Syria, huku Rais Bashar al-Assad akiapa kwamba kamwe waasi hawatashinda na mataifa ya Magharibi yakiilaumu Iran kuusaidia utawala wa Assad kwa silaha.
Zuma awataka wawekezaji wasiwe na wasi wasi
Afrika kusini tangu mwaka 2007 imekuwa miongoni mwa kile kinachojulikana kama washirika kumi wa kimkakati wa umoja wa Ulaya. Haya ni mataifa ambayo yanaumuhimu mkubwa kwa umoja wa Ulaya.
Marekani na Uingereza zamuonya Assad
Waziri Mkuu wa Uingereza na Rais wa Marekani wameonya kwamba wanaweza kulazimika kuchukua hatua nyingine mpya dhidi ya Syria, endapo taifa hilo litatishia kutumia silaha zake za kemikali katika mapambano yake na waasi
Uingereza yaapa kumkamata Assange
Mgogoro wa kidiplomasia unaendelea kati ya Uingereza na Ecuador huku polisi wa London wakivinjari nje ya ubalozi wa Equador kumkamata mwanzilishi wa WikiLeaks, Julian Assange, ambaye amepewa hifadhi na Equador.
Hatima ya hifadhi ya Julian Assange leo
Ecuador itatoa uamuzi leo juu ya kumpa hifadhi ya kisiasa mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks Julian Assange uamuzi ambao unaweza kusababisha mvutano wa kibalozi baina ya nchi hiyo na Uingereza.
Olimpiki 2012 :Malkia azindua rasmi
Mchezo wa kuogelea na mbio za baisikeli ndio vivutio vikubwa katika michezo ya Olimpiki hii leo Jumamosi (28.07.2012) mjini London mbali ya michezo mingine mbali mbali. Wanamichezo wakiwania medali za mwanzo.
Syria itatumia silaha za sumu ikishambuliwa
Syria imekiri leo(23.07.2012) kuwa ina silaha za kemikali na kuonya kuwa itazitumia iwapo itashambuliwa na mataifa ya nje, licha ya kuwa haitazitumia dhidi ya raia wake.
Urusi, China zalipigia kura ya veto azimio juu ya Syria
Urusi na China kwa pamoja zimelipigia kura ya veto azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililotaka kutumika kwa Ibara ya Saba ya Mkataba wa Umoja huo kuichukulia hatua kali Syria na kusitisha umwagaji damu.
Umoja wa Ulaya waipatia Uhispania Euro bilioni 30
Mawaziri wa fedha wa nchi zinazotumia sarafu ya euro wamekubaliana kuipatia Uhispania mkopo wa euro bilioni 30, kusaidia mabenki ya nchi hiyo ambayo kwa sasa yanakumbwa na mgogoro mkubwa wa kifedha.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya waanza mkutano
Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya wanakutana Brussels, Ubelgiji, kupitisha maamuzi juu ya mikakati ya kukuza uchumi. Hata hivyo kuna matumaini madogo tu ya kupatikana suluhisho la kupunguza madeni.
Malkia Elizabeth ziarani Irland Kaskazini
Malkia Elizabeth wa Uingereza kwa mara ya kwanza amekutana na kusalimiana kwa kupeyana mkono hii leo na kiongozi wa zamani wa kundi la wapiganaji wa IRA Martin McGuinness.
Msafara wa Balozi wa Uingereza Libya washambuliwa
Merkel apiga hatua ya muhimu katika mkutano wa G20
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameyapuuza maoni yaliyotolewa na wakosoaji juu ya mpango wake wa kuimarisha sarafu ya Euro. Merkel ameonyesha kuushikilia msimamo wake katika mkutano wa G20.
Ugiriki yapiga kura, euro mashakani
Wakati Wagiriki wakipiga kura leo (17.06.2012) katika uchaguzi unaoweza kuamua hatima ya taifa hilo katika sarafu ya euro, kushindwa kwa vyama vya kisiasa kutafuta msimamo wa pamoja kunaonyesha hali ya mtafaruku.
Uefa, Euro 2012; Uingereza na Ufaransa zapeta
Vigogo vya soka katika bara la Ulaya vilitoka jasho na kutumia ujuzi wao wote kuweza kufuzu katika michezo ya kundi D.Ufaransa iliizibua Ukraine kwa mabao 2-0,wakati Uingereza ikairarua Sweden kwa mabao 3-2.
Wahariri wa magazeti watoa maoni juu ya Ujerumani kuipa Israel nyambizi
Wahariri wa magazeti leo wanazungumzia juu ya mgogoro wa madeni barani Ulaya na suala la Ujerumani kuipa Israel nyambizi. Pia wanatoa maoni juu ya Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza.
Mkutano wa EU wakamilika bila muafaka wa hati za dhamana
Viongozi wa Umoja wa Ulaya walimaliza mkutano wao wa kilele mjini Brussels kwa kuchukua hatua muhimu za kutatua mgogoro wa kiuchumi barani humo, huku hofu ya Ugiriki kujiondoa katika kanda ya euro ikiongezeka
Mkuu wa Sera wa EU azuru Myanmar
Mkuu wa Sera za Umoja wa Ulaya Catherine Ashton yuko nchi Mynamr leo kwa lengo la kufungua ukurasa mpya wa mahusiano kufuatia ulegezaji wa vikwazo vilivyowekewa nchi hiyo unaotarajiwa kuimarisha uwekezaji nchini humo.
Umoja wa Ulaya wamuandalia vikwazo vingine Assad
Umoja wa Ulaya umesema umetayarisha vikwazo vipya dhidi ya utawala wa rais Assad, vinavyolenga kuudhoofisha zaidi usiendelee na ukandamizaji.
Uingereza na Ufaransa zailaumu Syria
Uingereza na Ufaransa zinaishutumu Syria kwa sababu haiufuati mpango wa amani ulioafikiwa. Leo, mapigano makali yaliyouwa watu kadhaa yameripotiwa nchini humo.
Mke wa Assad naye awekewa vikwazo
Umoja wa Ulaya umewawekea vikwazo vya kusafiri, na kuzuia mali zao zilizoko ndani ya nchi wanachama wa Umoja huo, jumla ya watu 12 wa karibu wa Rais Bashar Assad akiwemo Mkewe, Asma al Assad.
EURO bilioni 130 kwa Ugiriki
Hatimaye ugiriki imefanikiwa kushawishi sehemu kubwa ya wakopeshaji wake binafsi kukubali kupata hasara kubwa kwenye hati zao za mikopo, na hivyo kusafisha njia ya kupatiwa dhamana ya pili
Uganda: Kuchunguzwa kwa kampuni ya mafuta ya Uingereza ya Tullow
Baadhi ya wabunge nchini Uganda wameanza kukusanya saini kutoka kwa wabunge wenzao, raia na mashirika yasio ya kiserikali ili kushinikiza bunge la Uingereza kuchunguza kampuni ya mafuta ya uingereza yaTullow.
Uingereza yaongoza juhudi mpya kwa Somalia
Mkutano wa kimataifa kuhusu Somalia umeanza (23.02.2012) mjini London Uingereza, kujaribu kupata suluhisho kwa migogoro inayoikumba nchi hiyo ya pembe ya Afrika kwa zaidi ya miongo miwili.
17.02.2012
Deutsche-Welle:Uingereza itaitisha warsha kuhusu haki za binaadam nchini Libya,kuisaidia serikali ya mpito ikabiliane na vituko vya makundi ya waasi nchini humo.
China yasema iko tayari kuusadia Umoja wa Ulaya
China hat seine Bereitschaft bekräftigt, der Europäischen Union bei der Bekämpfung der Schuldenkrise
Ugiriki yaidhinisha hatua za kubana matumizi
Bunge la Ugiriki limeidhinisha hatua kali za kupunguza matumizi ya serikali katika juhudi ya kudhibiti uchumi wake unaoelekea kuporomoka.
31.01.2012
Deutsche Welle:Mchezaji wa kiungo wa Newcastle, Yohan Cabaye anaandamwa na shirikisho la kabumbu la Uingereza kwa kumpiga teke mmisri Adam El-Abd timu ya Brighton.
Umoja wa Ulaya wasema uchaguzi DRC ulikuwa na dosari nyingi
Kikundi cha wachunguzi wa Umoja wa Ulaya kimeongeza sauti yake kwenye shutuma zinazoongezeka kukosoa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mkutano mkuu wa Umoja wa Ulaya kuanza leo
Viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wanatafuta uungwaji mkono miongoni mwa viongozi wenzao wa jumuiya ya ulaya ili kutatua mgogoro wa madeni unaokumba jumuiya hiyo. Viongozi hao wanakutana kwa siku mbili kuanzia leo.
Ujerumani na Ufaransa zapendekeza mabadiliko ya mkataba wa EU
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa jana wamekubaliana mabadiliko kadhaa yenye lengo la kuinusuru sarafu ya euro na utekelezaji wa nidhamu ya matumizi miongoni mwa wanachama wa EU.
Mvzozo wa kidiplomasia Iran, Uingereza wazidi
Serikali ya Uingereza imewaondoa mabalozi wake wote nchini Iran na kuufunga ubalozi wake mjini Tehran, ikiwa ni kujibu kitendo cha kushambuliwa kwa ubalozi huo hapo Jumanne.
Hali ni shwari Uingereza baada ya polisi kumwagwa
Kuwapo na polisi wengi zaidi katika miji mikubwa ya Uingereza hadi sasa kumezuwia ghasia , kukiwa hakuna ripoti za ghasia usiku wa jana.
Ghasia zaendelea katika miji ya Uingereza
Vijana jana usiku walipabana na polisi katika miji tofauti nchini Uingereza,lakini mji mkuu London, hali ilikuwa shwari kwa kiasi fulani jana usiku,baada ya polisi zaidi kupelekwa kwa maelfu.
Ghasia Uingereza zaingia siku ya nne; hadi Manchester
Ghasia mbaya kabisa ambazo hazijawahi kutokea nchini Uingereza kwa miongo kadha sasa zimesambaa hadi mji wa Manchester na maeneo mengine ya kati nchini humo.
Kashfa ya simu yamuangusha mkuu wa polisi Uingereza
Kashfa ya kunasa mazungumzo ya simu ya kampuni News Corporation imemgharimu wadhifa wake mkuu wa polisi nchini Uingereza na kuzusha hofu Waziri Mkuu David Cameron, anavyolishughulikia suala hilo.
Bunge la Uingereza lamtaka Murdoch kutoinunua BSkyB
Bunge la Uingereza linatarajiwa kupitisha hoja binafasi ya chama kikuu cha upinzani Labour kumtaka Rupert Murdoch kujitoa kwenye zabuni ya ununuzi wa kituo cha utangazaji cha BskyB.
Ufaransa na Uingereza zaumana leo robo fainali
Fainali za kombe la dunia kwa wanawake zimeendelea hapa nchini Ujerumani katika robo fainali. Mahasimu wa jadi katika soka Ufaransa wanaonyeshana kazi na Uingereza ambapo wenyeji Ujerumani inakibarua na Japan.
Uingereza yatoka sare na Mexico
Hapo jana, siku ya pili ya michuano ya kombe la dunia la Soka la Wanawake, inayofanyika hapa Ujerumani, timu nne zilijimwaga uwanjani, Uingereza ikimenyana na Mexico wakati Japan ilipoikaba New Zealand.
Mgogoro wa Kifedha: Ugiriki ku moto, EU yagawika
Mawaziri wa fedha wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro wameshindwa kufikia makubaliano juu ya kuisaidia Ugiriki, huku Ugiriki kwenyewe maandamano yakipamba moto dhidi ya mpango wa Umoja wa Ulaya kuuokoa uchumi wa nchi hiyo
NATO na Uingereza zaijadili upya operesheni ya Libya
Ndege za NATO zimeendelea na mashambulizi yake mjini Tripoli, huku Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Fogh Anders Rasmussen, akikutana na viongozi wa serikali ya Uingereza kujadiliana operesheni yao ya wiki 11 sasa.
Uhamisho na usajili wa wachezaji Uingereza
Timu za ligi ya Uingereza zinatumia fedha nyingi kwa wachezaji chipukizi wa nyumbani katika kile kinachoonekana kuwa kuzinduka kwa timu hizo kutokana na ukweli uliopo
Obama ahutubia bunge la Uingereza
Rais Barack Obama wa Marekani amelihakikishia bara la Ulaya kuwa litaendelea kuwa sehemu muhimu katika sera za Marekani za mambo ya kigeni.
Kiongozi wa waasi wa Libya akutana na Waziri Mkuu wa Uingereza
Nchini Libya, Kanali Muammar Gaddafi anaripotiwa kuonekana kwenye televisheni ya taifa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha wiki mbili za mashambulio makali
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 42 wa 50
Ukurasa unaofuatia