BOSTON: Afghanistan yataka dhamana ya wafungwa wake
22 Mei 2005
Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amesema serikali yake inataka dhamana ya opresheni za kijeshi za Marekani nchini Afghanistan.Vile vile serikali yake ikabidhiwe wafungwa wote wa Afghanistan walio chini ya uangalizi wa Marekani.Karzai amesema hayo kufuatia madai mapya yaliochapishwa na gazeti la Kimarekani,New York Times kuhusika na ripoti ya siri ya jeshi la Marekani kuwa wafungwa waliteswa na wanajeshi wa Kimarekani.Ripoti hiyo inahusika na vitendo vilivyotokea mwaka 2002,yakitajwa mateso yaliosababisha vifo vya wafungwa wawili.Rais Karzai aliwasili Boston jumamosi jioni akiwa katika ziara yake ya mwanzo nchini Marekani tangu kuchaguliwa kwake kama rais wa Afghanistan.Ameahidi kuwa atakapokutana na maafisa wa Marekani ikiwa ni pamoja na rais George W.Bush vile vile,atalijadili suala la udhalilishaji wa wafungwa wa Afghanistan.