JamiiBosnia na Herzegovina
Bosnia yaadhimisha miaka 30 ya mauaji ya Srebrenica
8 Julai 2025Matangazo
Maandamano hayo yameanza leo mjini Sapna na yataelekea umbali wa kilomita 100 hadi katika kituo cha kumbukumbu ya mauaji ya Srebrenica huko Pontocari.
Wakati wa mauaji hayo yanayokumbukwa, mwaka 1995, zaidi ya wanaume na vijana 8,000 wa Kiislamu wa jamii ya Bosniak waliuawa karibu na mji wa Srebrenica katika vita vya Bosnia.
Siku ya mwisho ya maandamano itaadhimishwa kwa hafla maalumu na siku inayofuata yatafanyika maziko ya waathiriwa wapya waliotambuliwa wa mauaji hayo ya halaiki.