Bonn:Maonyesho ya sanaa.
21 Julai 2006Matangazo
Jumba la sanaa na maonyesho ya wazi lililopo Bonn limeanza kuonyesha mkusanyiko wa kazi za sanaa mkusanyaji maarufu, Guggenheim.
Maonyesho hayo yaliyoanzia leo yatamalizika ifikapoJanuary 7 mwaka ujao wa 2007.
Mkusanyiko wa jumla ya kazi za Guggenheim umehifadhiwa huko New York, Venice, Bilbao, Las Vegas na Berlin.
Aidha maonyesho hayo ya wazi yatawakilisha historia ya sanaa iliyoanzia mwishoni karne ya 19 hadi mwanzoni mwa karne ya ishirini.