JamiiUfaransa
Bomu la Vita vya Pili vya Dunia lagunduliwa Paris
7 Machi 2025Matangazo
Shirika la reli la Ufaransa limesema bomu hilo lilipatikana "katikati njia ya ya reli" huko Saint Denis, kituo ambacho hupita treni kadhaa za mwendo kasi ikiwa ni pamoja na ile ya Eurostar inayoelekea mjini London.
Soma pia:Macron afanya mkutano na Merz
Polisi walikuwa katika harakati za kulitegua bomu hilo.
Mabomu yatokanayo na Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia hugunduliwa mara kwa mara kote nchini Ufaransa na katika mataifa mengine ya Ulaya, lakini ni nadra sana kupatikana katika maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu.