Bolsonaro wa Brazil awekwa kifungo cha nyumbani
5 Agosti 2025Marekani, ambayo rais wake Donald Trump na mshirika mkubwa waBolsonaro, imelaani uamuzi huo wa mahakama, ikiuita usiofaa.
Tayari, Trump alishatangaza kuipandishia ushuru wa asilimia 50 Brazil, akipinga kushitakiwa kwa mshirika wake huyo.
Jaji Alexandre de Moraes anayesimamia kesi hiyo aliamua hapo jana kwamba Bolsonaro, mwenye umri wa miaka 70, amekiuka masharti aliyowekewa na mahakama hiyo kwa kusambaza taarifa zisizo sahihi kupitia watoto wake watatu ambao ni wabunge.
Uamuzi huo wa mahakamaunakuja siku moja baada ya maelfu ya wafuasi wa kamanda huyo wa zamani wa kijeshi kuandamana wakilitaka baraza la seneti kutangaza msamaha kwa kiongozi wao.
Waendesha mashitaka wanamshutumu Bolsonaro kwa kuongoza genge la wahalifu lililopanga kupinduwa matokeo ya uchaguzi, ikiwemo njama ya kumuua mshindani wake, rais wa sasa Lula da Silva, na Jaji de Moraes, baada ya kushindwa kwa kura chache kwenye uchaguzi wa mwaka 2022.