Bolsonaro alikuwa anapanga kukimbilia Argentina
21 Agosti 2025Matangazo
Kulingana na polisi, barua hiyo ilikuwa katika simu ya mkononi ya Bolsonaro mnamo Februari mwaka jana, siku mbili baada ya kushikiliwa kwa pasi yake ya usafiri.
Haikuwa wazi iwapo barua hiyo ilikuwa imeshatumiwa rais huyo wa Argentina tayari. Afisi ya Milei haikutoa jawabu ilipoulizwa kuhusiana na suala hilo.
Barua hiyo ni sehemu ya ripoti ya mwisho ya polisi wa Brazil iliyomtuhumu rasmi Bolsonaro na mwanawe, Eduardo kwa kula njama ya kutaka kuingilia kati kesi ambayo rais huyo wa zamani anatuhumiwa kwa kupanga mapinduzi.
Kesi hiyo itaanza kusikilizwa mwezi ujao wa Septemba.