Boko Haram waua watu 9 na kujeruhi wengine Nigeria
7 Julai 2025Mamlaka nchini Nigeria zimesema wanamgambo wa Boko Haram wamewaua watu 9 na kuwajeruhi wengine 4 kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Shambulio hilo limefanywa na wanamgambo hao wa Boko Haram katika eneo la Babagana Zulum linalokaliwa na watu wa jamii ya Malamu Fatori, gavana wa jimbo hilo amesema lakini bila kutaja kwamba ni lini shambulio hilo lilitokea.
Kuibuka tena kwa mashambulizi ya Boko Haram kumelitikisa eneo la kaskazini mwa Nigeria katika miezi ya hivi karibuni, ambapo waislamu hao wenye msimamo mkali wamekuwa wakishambulia mara kwa mara vituo vya kijeshi, kuvamia raia na kuongeza hofu ya uwezekano wa kurejea kwa enzi ya ukosefu wa usalama katika maeneo hayo.
Eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria limeshuhudia mamilioni ya watu wakiyakimbia makazi yao kufuatia matukio hayo.