Bogota:Rais Uribe aapishwa.
8 Agosti 2006Matangazo
Rais wa Colombia Alvaro Uribe ameapishwa leo kwa kipindi chake cha pili cha urais.
Katika sherehe za kuapishwa Uribe ameahidi kutafuta njia za amani na waasi wa mrengo wa kushoto na kumaliza miongo minne ya vita vya wenyewe kwa wenyewe katika taifa hilo.
Wakati huo huo Uribe amesema ataimarisha sheria kali za za usalama na kuondosha mauaji ya mara kwa mara ya Colombia na ongezeko la utekaji nyara.
Maelfu huuwawa ama kupotea kila mwaka kutukana na machafuko yanayofanywa na kundi kumbwa la Colombia linalojishughulisha na biashara ya Cocaine.
Nchi hiyo bado inabakia kuwa ni nambari moja duniani kwa uzalishaji wa dawa zisizo halali licha ya msaada wa mamilioni ya dola za Marekani wanazopata kama msaada ili kuachana na biashara hiyo.