BERLIN:Wabunge wa Ujerumani wakutana kwa mara ya mwisho kabla ya uchaguzi mkuu.
7 Septemba 2005Wabunge katika Bunge la Ujerumani-Bundestag- wamo katika kikao chao cha mwisho kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa tarehe 18.
Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder katika hutuba yake,ametetea rekodi nzuri ya uendeshaji wa serikali yake.Kansela amesema mkusanyiko wa mageuzi uliowekwa bayana na chama cha Social Democrats kwa ushirikiano na chama cha kijani kinachowaunga mkono,umeifanya Ujerumani kuelekea katika njia muafaka ya kuimarisha uchumi wake.
Nae Bibi Angela Merkel mgombea wa nafasi ya Ukansela kupitia chama cha Christian Democrats,ameeleza kuwa serikali ya Kansela Schröder imeshindwa kabisa kutekeleza majukumu yake.Amesema Ujerumani imekuwa katika kiwango cha chini cha kuimarisha uchumi tangu Bwana Schroeder alipochaguliwa kuwa Kansela miaka saba iliyopita.