BERLIN:Mripuko wa bomu nchini Afghanstan ulikuwa ajali asema waziri wa Ulinzi wa Ujerumani
27 Juni 2005Matangazo
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Peter Struck amesema mripuko wa bomu uliotokea huko Kunduz nchini Afghanstan ulikuwa ajali na wala sio shambulio lililofanywa kimakusudi.
Hata hivyo wachunguzi wa kijeshi wa Ujerumani wamekwenda nchini humo kuchunguza kiini cha mripuko huo uliosababisha kuwawa kwa wanajeshi wawili wa Ujerumani na waafghanstan watano.
Ujerumani ina wanajeshi zaidi ya elfu mbili nchini Afghanstan wa kulinda amani.