BERLIN:Miaka 50 ya jeshi la Ujerumani
27 Oktoba 2005Matangazo
Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa virungu na polisi mjini Berlin wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya jeshi la Ujerumani.
Watu hao waliandamana kupinga gwaride la kijeshi lililofanyika kwa ajili ya maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na waalikwa zaidi ya alfu tano ikiwa pamoja katibu mkuu wa jumuiya ya NATO Jaap de Hoop Scheffer .