BERLIN:Mgogoro wa kisiasa nchini Ujerumani
20 Septemba 2005Ujerumani inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa kufuatia matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika juzi ambapo vyama vyote vikuu viwili vilishindwa kupata kura za kutosha ili kuweza kuunda serikali.bila ya msaada wa vyama vingine
Vyama hivyo vikuu CDU na SDP vilipishana kwa kiasi kidogo sana na kila upande unadai kuwa na haki ya kuunda serikali.
Kila upande umetoa mwaliko kwa vyama vidogo vidogo ili kufanya mazungumzo juu ya kuunda serikali ya mseto.
Mwenyekiti wa chama cha CDU bi Angela Merkel amesema anakusudia kufanya mazungumzo na vyama vyote vingine juu ya hayo.
Katika hatua ambayo si ya kawaida katika mandhari ya kisiasa hapa nchini Ujerumani, bi Merkel ameonyesha utayarifu wa kukutana na wajumbe wa chama cha kijani.
.