BERLIN:Livni aiomba Ujerumani isaidie ili askari wa Isreal waachiwe
29 Agosti 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Israel bibi Zipi Livni ameiomba serikali ya Ujerumani isaidie katika juhudi za kuwezesha kuachiwa askari wawili wa Israel waliotekwa nyara na Hezbollah. Bibi Livni anaendelea na ziara nchini Ujerumani ameitaka Ujerumani iwasiliane na serikali ya Lebanon kwa ajili hiyo.
Wapiganaji wa Hezbollah bado wanawashikilia askari hao waliowateka kabla ya vita vya wiki nne kuanza nchini Lebanon.